Geoffrey alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mama Hassan ambaye alitoroka nyumbani majuma mawili yaliyopita.

"Mimi nilitoka kazi jioni na nikapata mke wangu amenuna na sikujua sababu na nikatoka na kwenda kumuona rafiki yangu fulani. Kurudi kwa nyumba sikumpata na nikapata watoto pekee yao na kila nikimpigia simu hajibu." Alisema Geoffrey.

Manze kazi ngumu ndugu yangu kuosha watoto na kuwapikia, naomba mnipatanishe."Aliongeza akidai hajui mkewe aliko lakini ana fununu kuwa yuko Kakamega.

Wawili hao wameoana kwa miaka kumi kwani walioana wakiwa wachanga sana.

"Wewe unajua nyumba ina kazi ngumu?" Mama Hassan alimuuliza mumewe akisema kuwa alitaka afanye hayo majukumu ili aelewe ugumu anaopitia.

"Mimi kutoka kwangu wewe mwenyewe si unajua? Pia wewe unaskiza mambo ya watu sana na unawaamini. Ulifanya track ya number yangu ulipata nini mbaya?" Aliuliza Beth.

Baada ya hayo yote Geoffrey alikiri kuwa aliskia tu fununu na alipojaribu kumfuata mkewe hakupata chochote kibaya.