Bwana William aliomba apatanishwe na mkewe bi Amina akidai kuwa wawili hao wamekosana kwa mda mrefu sasa.

"Bado hajaolewa kwani kuna siku tulizungumza na akadai kuwa angependa kurudi lakini dini yake ya kislamu ndio inamzuia kurudi.

Sahii amepata shida kwao na majirani wanasema kuwa nyumba imefungwa na watoto wangu wanahangaika na ndio maana naomba msaada." Alisimulia William.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na wamejaliwa na watoto wawili.

Kulingana na William, wawili hao wameishi kwa amani na juzi juzi ndio wazazi wa mkewe ndio walisema kuwa hawawezi olewa na kafiri.

"Nimekataa maneno yake sirudiani naye wacha nihangaike na watoto wangu. Huyu huniangaisha miaka nyingi hata babangu anajua kwani akinywa pombe huja kunivuruga kwa nyumba." Amina alisema akiwa na uchungu mwingi.

Amina alikana kuwa sio mambo ya dini iliyopelekea wao kutengana ila ni tabia zake, huku akisema kuwa alikuwa anamtusi mbele ya watoto wake.

"Juzi alinipigia simu akisema anataka kuoa bibi mwingine na nikamruhusu kwani niliona amefunguka akili." Alisema Amina ambaye hana nia ya kurudiana na aliyekuwa mumewe.