Asilimia 58 ya wanawake humu nchini hukumbana na unyanyasaji wanaposafiri kwa matatu kila siku.

Ripoti ya ufahamu wa kijinsia katika sekta ya uchukuzi iliyotolewa na shirika la Flone na lile la Makaazi ya binadamu la Umoja wa Mataifa (UN HABITAT) imefichua kua matamshi kuhusu miili ya wanawake, maneno ya ngono na kutomaswa ndio aina za unyanyasaji zilizokithiri mno.

Takriban asilimia 38 ya wanawake wanaofanya kazi katika sekta ya uchukuzi wanasema unyanyasaji kupitia maneno ya matusi ndio uliokithiri ikifuatiwa na kutomaswa kwa asilimia 32.  Wengine asilimia 15 walitaja kuitishwa fadhila za kingono na abiria,wahudumu polisi na wanachama wa sacco.

Asilimia 4 ya waliohojiwa walitaja aina zingine za unyanyasaji kama vile kuvuliwa nguo kwa wanawake hadharani huku asilimia 90 ya wahudumu wa kiume wakisema kua mavazi ya wanawake yanachangia unyanyasaji huo.

Ripoti hio inasema 'Ukosefu wa umani kwa idara za usalama na unyanyapaa dhidi ya waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono pamoja na ukosefu wa jitihada za usimamizi wa sacco za kuwawajibisha watekelezaji' ni sababu zinazowapelekea waathiriwa kutoripoti visa hivyo.

View Comments