DCI

Maafisa wa idara upelelezi DCI wameelekea Dubai kunakili taarifa kutoka kwa mwakilishi wa mtawala wa Milki za Kiarabu kuhusu sakata ya dhahabu yenye thamani ya shilling milioni 400.

Wapelelezi watamhoji Ali Zandi, mwakilishi wa Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum.

Zandi pia anawakilisha kampuni ya Zlivia inayojihusisha na biashara ya dhahabu na yenye makao yake Dubai. Dhahabu yake iliyopotea ilidaiwa kuzuiliwa uwanjani JKIA ikisafirishwa kutoka DRC kuelekea Dubai.

Zandi hufanya biashara kwa niaba ya Sheikh Maktoum na amekuwa Kenya mara kadhaa akifuatilia shehena yake, akiwa tayari amelipa mamilioni ya pesa kwa shehena ya kwanza.

Maktoum alimlalamikia rais Uhuru Kenyatta kuwa dhahabu yake ilikuwa imezuiliwa katika uwanja wa ndege wa JKIA kwa miezi kadhaa.

Wakati rais Kenyatta alipofanya uchunguzi alingudua kuwa hakukuwepo dhahabu kama hiyo na akaagiza msako dhidi ya wahusika.

Wapelelezi wameimarisha uchunguzi baada ya Kiongozi wa mashtaka ya umma Noordin Haji kumwagiza Inpekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai kuchunguza ripoti kuwa kundi Fulani la raia wa Kenya huenda walimlaghai Al Maktoun mamilioni ya pesa.

Polisi wana hadi Jumatano wiki ijayo kuwasilisha ripoti ya uchunguzi wao kwa Haji.

Wakiwa Dubai maafisa hao watajaribu kupata ushahidi wa kutosha zikiwemo sauti, stakabadhi, picha na video ili kutambua wahusika wote.

Punde tu watakapomaliza kuchukuwa taarifa kutoka kwa Zandi, polisi watawaita waliotajwa kuandikisha taarifa zao kabla ya kuwasilisha kesi dhidi yao na kuwakamata.

View Comments