Jacob, 29,  alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Atieno, 26, akidai wawili hao hukosana kila siku akidai kuwa kila siku anapotoka kazini yeye husema ametoka kwa mipango ya kando.

"Mama ulete shida kwani hata wasichana wa kazi wakinipigia yeye husema ni mamanzi nzangu. Nafanya kazi shuleni kwani mimi ni mwalimu na isitoshe amenivunjia simu karibu tatu." Alieleza Jacob.

Wawili hao wameoana kwa mda wa miaka mitano na wamejaliwa watoto wawili.

"Alikuwa anafanya kazi usiku na akanipigia simu niende anapofanya kazi, na asubuhi akaenda kazi akasahau wallet kwa nyumba na kuangalia nikapata condom.

Kumuuliza akadai kuwa ilikuwa ya nduguye na ilianguka na akamuekea hapo tukagombana na nikaondoka." Alisimulia Atieno.

Aliongeza akisema kuwa kuna mwanadada kwa jina Millicent alimpigia mumewe akimwambia wakutane Kondele na hapo akanyamaza. Isitoshe Atieno alipigiwa simu na Millicent akimtusi akidai kuwa mumewe alimuacha kitambo na atamuoa kama mke wa pili.

"Tulipoenda Kisumu mahala mume wangu anapofanyia kazi alianza kutongoza mfanyikazi." Aliongeza Atieno akisema kuwa mumewe ana tabia za mipango za kando.

Wawili hao walirushiana cheche za maneno lakini bwana Jacob aliahidi kubadilisha mienendo yake huku bi Atieno akimuonya kuwa kuna magonjwa mengi.

View Comments