Bahati ni mmoja wa wanamziki wenye utata katika sekta ya mziki wa injili ila hilo halijamzuia kusonga mbele ili kutimiza ndoto zake.

Miezi chache zimezopita sasa, baada ya wasanii kadhaa kuhama lebo yake ya kurekodi, EMB, huku wakimsingizia kuwa alikuwa anawadhulumu. Kati ya waliohama lebo hiyo ni Mr Seed na David Wonder aliyewadhania kuwa 'ndugu zake'.

Mr Seed alihama lebo hiyo kwa madai kuwa mke wake Bahati, Diana Marua, alikuwa amemuonyesha madharau mpenzi wake ambaye alikuwa anatarajia kujifungua mtoto. Tendo ambalo lilifanyika kwenye tamasha ya kuvuka mwaka.

Bahati alikiri kuwa alichukua wawili hawa chini ya lebo yake wakati walikuwa wanahitaji msaada wake. Bahati alikiri kuwa hakuongelea swala hilo kwa sababu Mungu anapokea tu sifa. Bahati yu tayari kupokea msamaha wao wakiwa tayari kuuomba kwani msanii mmoja,Wisdom, tayari amemuomba msamaha.

Bahati alifunguka pia katika harakati ya kuwapa wasanii hawa msaada, lebo yake ya rekodi ilipoteza takribani shilingi milioni sita kwa muda wa miaka mbili.

Alisema haya;

''Nilipoteza shilingi milioni sita katika harakati ya kusimamia wasanii wangu na kujaribu kufanya miradi. Nyimbo moja ingenigharimu kati ya shilingi elfu mia nne na hamsini na shilingi elfu mia tano lakini mazao yangekuwa machache sana, lakini ni sawa. Katika harakati hii yote nilitumia pesa nyingi sana.''

Bahati aliwasihi mashabiki wasiwe wepesi wa kukimbia kwenye mitandao na kumsuta kwani hawajui ni yapi huendelea kabla ya mziki kamili kuisha na kuwekwa kwenye mitandao. Alisema kuwa hana deni ya mtu yeyote kwani ikiwa kungekuwa na deni angekuwa kortini tayari.

''Siwezi enda kwenye mitandao ya kijamii na kujibizana na mashabiki kwa kuwa hawaelewi mziki ni bei ghali sana. Imenibidi kuwa mtu mzima kwa suala hili kwa kufyata ndimi langu,'' alisema Bahati.

Alizungumza haya katika sherehe ya kuzaliwa tena kwa rekodi yake ya EMB ambayo ilifanyika kwenye jumba la KICC. Aliwaalika rafiki zake na familia ambao walikuwa wakimuunga mkono tangu atoe wimbo wake wa kwanza, Mama.

Bahati aliweka wazi kuwa usiku huo haukuwa tu kuhusu mlo, bali ilikuwa ni sherehe ya kurudisha mkono kwa wale waliomuunga mkono kwa kila jambo alilofanya.

View Comments