D8IOVV2WsAUayX5.jfif

Serikali imetangaza Jumatano, Juni tarehe 5, siku kuu ya kitaifa kuadhimisha siku kuu ya Idd-ul-Ftr, kuashiria kumalizika kwa mwezi mtukufu wa ramadhan kwa Waislamu.

Kupitia ilani katika gazetu rasmi la serikali la Juni tarehe 3, waziri wa Usalama wa ndani Fred Matiang’i alisema siku hiyo itakuwa kwa heshima ya Ramadhan.

Waziri alisema wakenya wote watajiunga na Waislamu kuadhimisha siku hiyo.

Mwezi mtukufu kwa waislamu ulianza Mei 5, na utakamilika Juni 4.

View Comments