Iwapo una noti nyingi za 1000   hautahitaji kuwa na akaunti ya benki ili kuzibadilisha na noti mpya za kisasa . Gavana wa  Benki kuu  Patrick Njoroge   amesema utahitaji tu kutemebelea benki yoyote iliyo karibu nawe  ili kuzibadilisha na noti mpya.

Hata hivyo amesema lazima anayezibadilisha notyo hizo za kale na mpya aweze kujitambulisha na kuthibitsha kwamb apesa hizo ni zake kihalali . Noti za shilingi 1000 hazitakubaliwa baada ya Oktoba tarehe moja .

Njoroge  amesema wale walio na kati ya shilingi milioni moja na  milioni tano za  shilingi 1000 watalazimika kutremebelea benki  ambazo wana akaunti ili kuzibadilisha na waeleze walivyozipata pesa hizo ili kubadilishiwa na noti mpya .

View Comments