Seneta wa Lamu Anwar Loitiptip amepata afueni baada ya kupitisha masaa kadhaa kwenye chumba cha wagonjwa hali mahututi, baada ya kushambuliwa eneo moja la burudani Kasarani.

Anwar alikuwa pamoja na mtoto wa gavana wa Nairobi Mike Sonko, Saumu Mbuvi.

Wawili hawa wamechumbiana.

Anwar aliyekuwa anaongea akiwa hospitali ya Aga Khan alisimulia jinsi wanaume walimshambulia Saumu huku wakiwa kwenye mazingira ya klabu.

''TULIKUWA NDANI YA GARI MAHALA PA KUEGESHA MAGARI KABLA YA MCHUMBA WANGU (SAUMU) KUTAKA KUENDA KWENYE CHUMBA CHA KUJISAIDIA. ALIPOFIKA HAPO, WANAUME WAWILI WALIMFUATA NA KUFUNGA MLANGO. WALIRARUA BLAUSI YAKE NA KUTAKA KUMBAKA. ALIOMBA USAIDIZI.''

Hapo ndipo Anwar alitoka kwenye gari na kukimbia kwa usaidizi wake. Alirusha jiwe kwenye chumba hicho cha kujisaidia ili kuwapa hofu. Walifungua mlango na kumuacha Saumu huru.

''WALITOKA INJE HUKU WAKIOMBA MSAMAHA WAKISEMA 'HATUKUTAKA KUFANYA LOLOTE'. NILITAKA KUTUMIA NGUVU LAKINI SAUMU ALINITULIZA KWA KUSEMA, TUNAWEZA KUWA VICHWA VYA VYOMBO VYA HABARI KWA KUPIGANA.''

Aliendelea kusimulia jinsi shambulio hilo lilitekelezwa na wanaume wengine wanaoaminika kuwa na mahusiano na wale waliojaribu kumbaka Saumu.

''Baadae, mwamaume mmoja aliyekuwa amebeba rungu na kipande cha chuma aliungwa na wengine kama sita hivi. Papo hapo walinipiga mara kadhaa kwa kichwa. Tangia hapo sikumbuki kitu yoyote hadi nilipoamka nikajiapata hospitalini.

Seneta huyu kijana aliongeza kuwa kitu kilichokwama akilini kutokana na shambulio hilo katili ni mazungumzo yake na wavamiaji hao.

''KITU TU NINACHO KUMBUKA NI WALIVYONIAMBIA. WALISEMA, 'HATUTAKUWACHA UKIWA HAI. UTAJUA SISI NI NANI'. KUSEMA UKWELI SIJUI KUSUDI LAO LILIKUWA GANI KWA KUWA WALINIWEKA MAJERAHA TU KICHWANI.''

Uchunguzi wa polisi unaendelea.

View Comments