BigEye.UG

Nikama imekuwa mtindo kwa wasanii mashuhuri kutoka Uganda kujitosa kwenye siasa.

Bobi Wine amejipata kwenye utata wa kisiasa tangia awanie kiti cha ubunge mwaka wa 2017.

Sasa, msanii, Jose Chameleone, ama ukipenda Joseph Mayanja, ametangaza kuwa atawania kiti cha umeya cha mji mkuu wa Kampala, baada ya kunukuliwa na gazeti la Uganda's Observer.

Chameleone ni mmoja wa wasanii wakuu Afrika mashariki. Moja ya nyimbo zake ambazo zinatumbulika ni Shida za Dunia wimbo ambao unazungumzia magumu wananchi wanazopitia.

Akielezea malengo yake, alisema:

 "Wakati huduma katika nchi zinafeli, wananchi huanza kuamka ... watu wameanza kutamani uongozi unaotosheleza na kufikia sasa bado haujafanikishwa".

Chameleone anatambua ushawishi wake Bobi Wine.

"Wenye wanafikiria nimesisimuliwa na Bobi Wine pia wana haki." Ananukuliwa akisema.

Bobi Wine alipiga kengele na kusema 'Tumekomaa sasa; twaweza fanya hili'. Nini mbaya na hilo? Kila kitu duniani kilianzishwa na mtu. 

Bobi Wine ambaye jina lake la ki serikali ni, Robert Kyagulanyi, alichaguliwa kama mbunge akiwa mwaniaji huru mwaka wa 2017.

Tangia alipochaguliwa, ameongoza maandamano kadhaa ambayo yamepelekea yeye kutiwa mbaroni na kushtakiwa na usaliti.

Alisema kuwa alipigwa na polisi alipokuwa gerezani.