st.stevens

Mwanafunzi wa kidato cha pili ambaye alitoweka kutoka shule ya upili ya wasichana ya St Stevens, Machakos amepatikana.

Msichana huyo wa miaka 16 alijitokeza nyumbani kwao, Kawangware, jana mchana baada ya kukosekana kwa mda wa miezi mitatu baada ya kutumwa nyumbani kuendea karo.

Mamake mwanadada huyo, Mary Mukami, amekuwa akimtafuta kwa miezi mitatu iliyopita bila mafanikio na hapo akawauliza wanahabari waandamane naye hadi shule ya mwanawe ili apate majibu.

Lakini walipofika shuleni, Mukami anasema kuwa alitambua kuwa mwanawe alikuwa ametumwa nyumbani kwa sababu ya kutolipa karo, habari ambazo alipata kutoka kwa marafiki wa mwanawe, na ambazo zilidhibitishwa na mwanawe.

Siku ya Jumatatu, wanahabari watatu kutoka stesheni ya KTN walivamiwa ndani ya shule hiyo walipoelekea kutafuta majibu kuhusu kukosekana kwa mwanadada huyo.

Shule hiyo hata hivyo imefungwa kwa sasa.

-Cyrus Ombati

View Comments