- africa_kenya_lake_nakuru_gallery_flamingos(1)
- Madaraka holiday destinatations

Kenya ni mojaapo ya sehemu za kuvutia sana ulimwenguni .Nchi hii haina upungufu  wa mambo unayoweza kufanya  au kuona .

Kutoka   taswira ya kipekee jua linapotua ,mbuga kadhaa  za wanyama na  mvuto wa  maporomoko ya maji.kutoka milima ,na maziwa ya kuvutia ,fuo za bahari  ,visiwa miongoni mwa vingine ,kenya ni jungu la kila unachoweza kutaka kutazama .

Tuangalie baadhi ya sehemu ambazo unafaa kuzuru nchini kenya .

Pwani

Pwani ,ina historia ya kipekee na asili na ni ngome ya wa mijikenda na waswahili .

Sehemu hii ndio tisha ya kuburudika na  kupumzika .mvuto wake hauna ubishi  !utaweza kuwashuhudia ngamia wakitembea pembeni mwa ufuo wa bahari  .maji yenye rangi ya samawati kwa mbali pia yanakupa picha itakayodumu fikrani kwa muda  .

Watalii wengi kutoka sehemu mbali mbali za dunia huzuru  eneo hili.

Maasai Mara

Mbuga ya kitaifa Maasai mara, ina wanyama wengi wa porini  unaoweza kuwatazama na kujifurahisha .

utapata fursa ya kutangamana na hali halisi asili ya abara la afrika . utashuhudia ujasiri wa jamii zinazopakana na mbuga hii kama vile masaai  ambao wamelelewa karibu na wanyama wa porini . Kuna Soga kwamba lazima  wapigane na simba ili wawe 'wanaume'

Lake Naivasha

Ni mto wa maji yasio na chumvi   nchini kenya na una maeneo bora sana ya kuweza kutawama  wanya wa pori . utaweza kuwaona ndege wa flamingo  wakiwa katika makaazi yao asili . unaweza kuwakaribia na kutangamana na wanyama kama vile chui , kifaru .

Mount Kenya

ni watu wachache duniani wameukwea mlima huu na wale waliofanya hivyo watakuambia una  mandhari  mazuri sana  ya kuvutia . itakulazimu ujionee mwenyewe ili uweze kunufaika na mazuri yote katika Mlima huu .

Giraffe Centre

The Giraffe Center  kipo mtaani Lang'ata kilomita 20 kutoka katikati wa jiji la Nairobi . kituo hiku kilianzishwa ili kuwalinda  twiga ambao maisha yao yalikuwa hatarini afrika mashariki .

utaruhusiwa kuwa;lisga twiga hawa  .Ni warefu sana utaweza kuwalisha ukiwa ndani ya hoteli  ,unapoteremsha kiamsha kinywa .

Nairobi National Museum

Makavazi  haya yanalenga kulinda utamaduni na turathi za kenya  kando na kuwapa wageni fursa ya kufahamu historia na  urithi wetu . kando na hayo wageni pia wana fursa ya kununua vitu na vyakula vya kipekee pamoja na kuzuru  bustani  zenye mimea  inayokupa  mandhari ya kipekee

Lamu Island

KISIWA cha Lamu kipo katika pwani ya kenya . kisiwa hiki  kinafikiwa kwa usafiri wa boti  hadi Mokowe  na pia hadi kisiwa cha Manda ,ambapo kuna uwanja  mdogo wa ndege .   kina mvuto  usioridhisha na hasa kwa wageni .

View Comments