Willy alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Amina au mama Ingolo, akikiri kuwa anaumia sana.

Tulikosana mwezi uliopita kwani tulianza kukosana mwaka uliopita.

Kabla nimuoe, nilikuwa na mwanadada mwingine ambaye tulipata mtoto pamoja na tukatengana. Sasa baada ya mtoto kufikia miaka mitano yule mwanadada akaanza kurudi polepole na kuanzisha urafiki na mamangu.

Alisema akiongeza,

Kisha ilifika wakati nikawa na mpango wa Kando ila hakuna kitu tulikuwa tunafanya ilikuwa tu ubeste lakini mke wangu alihisi ni mpango wa Kando.

Mwezi uliopita kulikuwa na mkasa wa moto na mali yetu yote ikachomoka na hapo akasema kuwa tuko vyenye tulipatana na sasa itabidi tutengane.

Bwana willy anasema hapo ndipo mkewe aliondoka na kwenda kwa dadake.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minane.

Bi Amina alipopigiwa simu, alikatiza mawasiliamo  kati yetu pindi tu aliposkia sauti ya mumewe.

"Mimi Gidi nishamsamehe lakini kurudiana naye nimekataa" Alisema Amina alipokubali kuwasiliana nasi.

Unikome! Na tena Sina haja na wewe na utafute bibi mwingine sio kila wakati kunipigia simu.

Utapata tu bibi mzuri ambaye mamako anapenda au uoe watu wa kwenyu. Aliongeza Amina huku akiwa na hasira chungu nzima.