musaliamudavadiandrashidechesa

Aliyekuwa waziri wa michezo Rashid Echesa na seneta wa Kakamega Cleophas Malala wametangaza kuzika tofauti zao na kumuunga mkono kinara wa ANC Musalia Mudavadi katika azima ya kuwania urais mwaka alfu mbili ishirini na mbili.

Wakihutubu eneo la mung’ang’a kwenye mazishi ya mama jesca wamatsi mamake mwanansiasa wa anc mumias mashariki David Wamatsi, Echesa ambaye amekuwa mwendani wa naibu wa rais William Ruto, na Malala ambaye ni mwendani wa kinara wa ODM Raila Odinga, wamesema ni wakati wa jamii ya waluhya kukwamua heshima yao kwa kuungana na kuitisha uungwaji mkono kutoka kwa jamii zingine.

Kwa upande wake Mudavadi amepongeza hatua hiyo na kushikilia kwamba amewasaidia viongozi kutoka maeneo mengine vya kutosha na ni wakati sasa warudishe mkono.

View Comments