crimesceneistock000020049073bradcalkins(2)

Shule moja ya msingi katika kaunti ya Homa Bay , Suba kusini imegumbikwa na wingu la simanzi baada ya mwanafunzi wa darasa la pili kumuua mwenzake wakicheza uwanjani.

Collins Onyango, 9, alifariki akipata matibabu katika zahanati ya Seka jumatatu alasiri. Wawili hao walikuwa wakicheza kirafiki kabla wakosane. Mwanafunzi aliyemzidi kwa umri alimsukuma kwa ukuta akitumia nguvu.

Mwelekezi wa ujajusi kaunti ya Homa Bay Daniel Wachira amesema kuwa mshukiwa hatashtakiwa kwa kosa la mauaji.

"Wazazi wa mwanafunzi aliyeafariki wamejuzwa kuhusu kifo cha mwanao." alisema Wachira. 

Wazazi waliofiwa wamesema kuwa hawatamshtaki yeyote kwani muuaji ana umri mdogo.

Hadithi imehaririwa na kuchapishwa na Abraham Kivuva

View Comments