- state house
- kenyatta.national.hospital
- State_House_Nairobi

Msemaji wa ikulu Kanze Dena ameonya kuwa ni hatia kupenyeza katika maeneo yaliyotengwa kwa umma.

Hii ni baada ya tukio la jana jumatatu wakati kijana mmoja wa makamo  kupigwa risasi katika jaribio la kuingia maeneo yale.

"Tunachukua nafasi hii kuwakumbusha  wananchi kuwa ikulu ni pahala palipotengwa. Kwa hivyo, mtu yeyote hapaswi kuingia humu bila idhini ya mamlaka husika." alisema Kanze.

Soma hapa:

Brian Kibet Bera,25 ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha JKUAT alipigwa risasi jumatatu na polisi waliokuwa wakishika doria nje ya ikulu.

Kijana huyu wa makamo alipanda moja ya lango kuu za ikulu na kuingia ndani. Polisi walimwandama ili ajisalimishe na kilichowashangaza akakichomoa kisu jambo na ambalo lilifuatia kupigwa risasi na kupata jeraha.

Kisa hiki kilifanyika saa kumi na dakika tano jioni na mshukiwa kufikishwa katika kituo cha polisi Kileleshwa na kusajiliwa katika kitabu cha matukio OB nambari 39 baadaye akapelekwa katika hospitali ya kuu ya Kenyatta kwa matibabu.

Soma hapa pia:

Ikulu imetangaza kuwa upelelezi unafanyika kubaini kiini na azimio la mshukiwa kupenyeza katika uwanja wa ikulu huku likionya kuwa hatua ifaayo itakuchukuliwa baada ya kukamilisha zoezi nzima.

View Comments