12 June 2019 1 Min Read
Mvulana aliyekuwa na ebola Uganda afariki
by Yusuf Juma Habari
Mtoto mvulana mwenye umri wa miaka mitano aliyekuwa na kisa cha kwanza kilichothibitishwa cha ebola nchini Uganda ameaga dunia . Mtoto huyo alikuwa akipokea matibabu katika kituo cha matibabu ya ebola huko Kasese karibu na mpaka wa Uganda na Jamhuru ya Kidemokrasia ya Congo .
Shirika la afya duniani WHO jana lilithibitisha kwamba kisa cha kwanza cha ebola nchini Uganda Kilitokea DRC ambako mchipuko wa ugonjwa huo hatari umeripotiwa .
Familia ya mtoto huyo ilikuwa imesafiri hadi DRC kuhudhuria maazishi na kurejea Uganda tarehe 9 juni .Alipelekwa hospitali akiwa na daalili za virusi vya ebola