- 1324
- Mike-Sonko-II-470x264
- unnamed (8)

Gavana wa kaunti ya Nairobi, Mike Mbuvi Sonko anahofia usalama wa maisha yake. Sonko anasema kuwa kuna watu serikalini ambao wana nia mbaya ya kumtoa uhai. Gavana huyu anadai kuwa kuna ndege aina ya drone inayozunguka karibu na ofisi yake Upperhill ili kuchunguza aendapo. Kulingana na Mike, ndege hii ina kamera zinazotumika kunasa achokifanya.

Soma hapa:

Tazama chapisho lake katika mtandao wa Facebook:

Gavana huyu anahofia kuwa huenda hasimu wake wa kisiasa katika serikali ya Jubilee wanataka kumwangamiza. Sonko anawashtumu tawi maalum la wanapolisi kuwa wanapanga njama hiyo.

Habari hizi zinachipuka muda tu baada ya kuhusika katika mgogoro na mwakilishi wa wanawake kaunti ya Nairobi Esther Passaris.