Mwanamke mwenye umri wa miaka 27 anauguza majeraha katika  hospitali moja ya kibinafsi huko Mwea ,Kirinyaga baada ya kuchomwa na mumewe kwa kumpikia Githeri badala ya wali .

Kwa mujibu wa shangazi yake mwathiriwa , Peter Ngugi mwenye umri wa miaka 32  alihamakishwa na hatua hiyo na kumtupia mkewe stovu iliyokuwa ikiwaka .OCPD Lucas Chebet amesema mshukiwa  anasakwa ili kukamatwa na atafikishwa kortini . wawili hao wamekuwa katika ndoa kwa miaka miwili na wana watoto wawili .

View Comments