biskuti za bangi

  Polisi huko Thika  wamewakamata wanafunzi wawili wa chuo kikuu cha (KCA)  waliobatikana wakizioka biskuti zilizotiwa bangi .John Gitonga na  Robert Ndee were walikamatwa katika nyumba yao mtaani Githurai Kimbo  walipokuwa wakizitayarisha bisikuti hizo .

Kamanda wa polisi Kiambu  Ali Nuno  amesema walipewa habari na wananchi kuhusu shughuli za wanafunzi hao  kisha wakafanya oparesheni ya kuvamia nyumbao waliokuwemo . wawili hao walikuwa wamesaga bangi na kuichanganya na unga uliotumiwa kuoka biskuti . Wawili hao yaonekana walikuwa na wateja wengi kwani biashara hiyo imekuwa ikifanyika kwa muda mrefu .

Nuno amesema wanafunzi hao wamekuwa wakiziuza biskuti zao  kwa wanafunzi wenzao . Bangi iliyosagwa na kuwa unga ,unga wa ngano na vifaa vya kupika  vitamu  hivyo vilipatikana katika nyumba ya washukiwa .Mmoja wa wanafunzi hao anasomea  Uhandisi .

 

View Comments