- 160725165907-kofi-olomide-performing-large-169
- editor594634055701458020
- file_57947cf56f6c4__1561029499_99698
- koffi 2

Staa na fundi wa muziki kutoka nchi ya Afrika ya kati Kongo, Koffi Olomide amepata pigo baada ya fiesta zake mbili kufutiliwa mbali Afrika Kusini. Tamasha hizi mbili zilikuwa zimepaniwa kufanyika tarehe 28 mwezi huu Shimmy Beach Club na Gallagher Convention Centre mjini Cape Town.

Soma hii:

Kufungiwa kwake kutumbuiza nchini humo kuna misingi ya kuhusika katika skendo ya ubakaji ya mojawapo wa madensa wake aliye na umri wa miaka 15. Koffi ana historia ya kuwapiga na kuwajeruhi watu katika fiesta. Mwaka wa 2008, staa huyu alituhumiwa kumpiga teke mpiga picha wake nchini Kinshasa.

Msanii huyu aliwahi kufurushwa humu nchini baada ya kunaswa katika video akimpiga teke densa wake katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).

Soma hadithi nyingine hapa:

Kampeni za kupinga tamasha zake staa huyu wa Kongo zilianza katika mitandao ya kijamii. Hii ilipelekea mkurugenzi mkuu wa Convention centre  Charles Wilson kutoa taarifa kuwa hataweza kuwakonga nafsi mashabiki wake katika ukumbi huo.

"Tafadhali mnafahamishwa kuwa onyesho la Koffi Olomide halitafanyika humu." alisema Charles.

View Comments