- najmbi-actress
- njambi6-640x360

Kila mtu hutamani mwonekano freshi wa mwili wake anapoishi na kutangamana na wenzake duniani. Muigizaji wa filamu wa kikundi cha Real House Helps of Kawangware Njambi amechapisha picha katika mtandao wake wa instagram na kuonyesha zama zile akiwa na tumbo laini.

"That one time I had a flat tummy..... Believe me I was flaunting it....😜😜..... In short nothing lasts forever." 

Tazama hapa:

https://www.instagram.com/p/BypBcCFnJfi/

Soma hadithi tofauti:

Kwa picha za wakati huu muigizaji huyu anaonekana na utambi japo sio kwa sana. Mabinti wengi katika uigizaji hujali sana mwonekano wao wanapotokea katika kazi zao za sanaa. Kunenepa mwili kwa wakati mwingine kunaweza sababishwa na kuzaa kwa wanawake au labda lishe.

Katika mahojiano na Word Is, mrembo huyu alifunguka mwanzo mwisho jinsi walivyotengana na mpenzi wake wa awali. Njambi anadokeza kuwa walikuwa hawajakua bado na kwa hivyo mara kwa mara kulikuwepo na majaribu ya kuchepuka.

Soma hadithi nyingine:

Njambi aliongeza kuwa kwa sasa wapo freshi na wanasaidiana katika malezi ya mtoto wao. Muigizaji huyu aliweka pembeni taaluma yake ya mwanasheria na kuzamia ndoto yake ya kuigiza katika filamu.

View Comments