- kimanyano
- boni
- boniface kimanyano

Boniface Kimanyano ndiye alikuwa mgeni wetu siku ya Jumanne katika kitengo cha Ilikujae, naye Massawe Japanni.

Stori yake Kimanyano ni ya kutisha, ya kushangaza na pia ya kumpa mtu moyo kwani baada ya miaka kumi na minane ya uhalifu na kutumia mihadarati, mwishowe alibadilika na sasa yeye ndiye huwashauri vijana dhidi ya kuingilia maisha aliyoishi.

Kulingana na Boniface ambaye ni kifungua mimba katika familia ya watoto saba, alianza uhalifu akiwa mchanga mno kwani tabia yake ya kuwa na kichwa ngumu ilimpelekea kufukuzwa shuleni akiwa darasa la nane.

Nilianza nikiwa chuo, kupiga watoi chuo, matusi na kuendelea hivyo nikachujwa shule nikiwa class 8. Hapo mathe naye alinifukuza nyumbani nikiwa na miaka 14. Alisema Boni.

Aliongeza,

Niliingia kwa streets na kule nikaanza kutumia madawa kama gum, yellow, blue Mercedes na nilikuwa na survive makaburini huko lang'ata.

Baada ya kufanya uhalifu wa kuibia watu simu na fedha, Boniface alijipata ameingizwa katika biashara ya kukata wanawake matiti ambazo anasema zilimletea fedha nyingi.

Anasema kuwa kazi yake ilikuwa kuteka wasichana kwa kuwawekea madawa na kisha kuwakata titi la upande wa kulia ila sio kushoto ili kuzuia vifo.

Kisha alikuwa anatuma ujumbe kwa mnunuzi akiwa bustani la Jeevanjee akisema amekamilisha kazi yake na kisha kuondoka. Yule mnunuzi akihakikisha kuwa amepokea alikuwa anamtuma mahala ambapo alikuwa anachukua malipo yake.

Anasema kuwa lengo lilikuwa kukata matiti makubwa kwani hayo ndiyo yalikuwa na malipo haba. Alifichua kuwa amewahi lipwa shilingi 140,000 katika biashara hiyo.

Matiti ilikuwa na pesa, nilikuwa napigiwa simu na kuangalia simu unaona umetumiwa elfu 30. Nilikuwa nawekea wanawake haswa makahaba madawa.

Ukibonga naye ile dawa nimeweka kwa kucha na nikimpitishia kwa mapua anapoteza fahamu na namweka kwa teksi, ikifika mahali nabaki naye nakata matiti ya upande wa kulia kwani ya kushoto anaweza fariki.

Nilikata wanawake watatu kabla ya kuwacha.

Boniface sasa ni baba wa wanadada wawili mapacha alifichua kuwa ana kibarua cha kuwalea wana wake pekee yake baada ya mkewe kutoweka.

Alisimulia jinsi kesi hiyo ilipofika kortini jaji alimpa majukumu ya kuwalea wana wake baada ya mkewe kufika kortini akiwa mlevi huku akitafuna miraa.

Mke wangu alikuwa mlevi sana na hakuwa anashughulikia watoto na tulipoenda kwa jaji alisema kuwa nafaa kuwatunza kwani mke wangu alikuwa anakula miraa na alikuwa mlevi ajabu.

Anasema kilichopelekea kubadilika kwake ni baada ya kushuhudia jinsi marafiki zake walikuwa wanauwawa. Isitoshe wao hao ndio waliomtokezea kwa ndoto na kumshauri kuwacha uhalifu.

Ilifika mahali nikaona nimebaki pekee yangu baada ya marafiki zangu kuuliwa na walikuwa wananikujia na kuniongelesha kwa ndoto zangu na hapo nikaamua kubadilika.