26 June 2019 1 Min Read
Diamond Platinumz ataja siku ya harusi
by Albanus Kiswili Habari
Diamond platinumz amefichua siku anayo pania kumuoa mpenziiwe Tanasha.
Akizungumza na waandishi wa habari wa lebo yake ya Wasafi, katika wasafi festivals kule mjini Dar - es- salaam jana, Diamond alisema huenda siku ya harusi yake na Tanasha ni tarehe 7 Julai mwaka huu.
Staa huyu wa kibao cha kanyanga na African Beauty, alisema kuwa sababu ya kupeleka harusi yake mbele kutoka tarehe 14 mwezi Februali mwaka huu ni kuwa hawakuwa wamejiandaa vyema kwa ajili ya hafla hio ya kiheshima ambayo inatarajiwa kuhudhuriwa na mastaa wengi wa nguvu ulimwenguni.