Kambua amesimulia jinsi mamake alivyomsaidia kumaliza chunusi usoni mwake katika mtandaso wake wa instagram. Kumaliza chunusi sio jambo rahisi kwani kulingana naye kambua ambaye hali hii ilianza kumuathiri akiwa katika shule ya upili.
Anasema kwamba aliang'ang'ana na hali hii kwa muda mrefu.

"Nilijaribu vitu vingi, vingine vya kununua kwa bei ghali huku vingine vikiwa ni maagizo kutoka kwa daktari wa ngozi, 'dermatologist' ila hakuna lolote lililobadilisha hali yangu ya uso.

Sikuyapenda maswali ya watu huku pia ushauri wao nikiuona kuwa hauna maana kwangu."

 Kambua mbaye ni mjamzito kwa sasa anasimulia kuwa hali hii hushusha ujasiri wa mtu. Hatahivyo mamake mzazi ndiye aliye mpa suluhisho kamili ya hali yake."

lazima niseme kweli kuwa chunusi hushusha ujasiri wa mtu. Mwaka uliopita nilikua kwenye studioni na rafiki yangu Gasheri aliniandikia ujumbe mfupi akiniuliza kama ningetaka kujaribu jambo lingine; @shethnaturals."

"Nilianza kutumia sabuni ya manjano kuosha uso, aloe vera kabla sijalala , rose water na mafuta ya Marula kuzuia uso usikauke."

"Baada ya kutumia hivo vifaa kwa muda mdogo uso wangu ulianza kubadilika," ukimwangalia Kambua utamshangaa jinsi uso wake ulivyo badilika. Anasimulia kuwa hivyo vimekuwa vifaa vyake kila siku na sasa hali ni shwari usoni mwake.