- rbggh
- bob-colymore-moments10-696x464

Wasanii nchini wametokea na kuwa katika mstari wa kwanza kumpa risala za rambirambi marehemu Bob Collymore. King Kaka,Brenda Wairimu,  na Akothee wamechapisha jumbe katika kurasa zao za insta wakiipa familia ya kiongozi huyu pole.

https://www.instagram.com/p/BzXSiNuI8sd/

https://www.instagram.com/p/BzXNDtXFAZj/

Soma hadithi nyingine:

Bob amekuwa akiugua ugonjwa wa saratani kwa muda mrefu. Jeff Koinange amesimulia jinsi walivyokuwa katika hali freshi na mlahaka mwema na familia ya mwendazake. Mtangazaji huyu ameweza pia kusema kuwa kifo chake walikuwa wanakitarajia.

Katika mahojiano na kituo cha utangazaji chini, staa huyu amedokeza kuwa Bob alikuwa tayari kufariki muda wowote. Madaktari wake walikuwa washawataarif ndugu na jamaa kuwa Bob huenda akaiaga dunia. Hii ni kufuatia afya yake ambayo ilikuwa inadorora kila uchao.

“Alitueleza tukiwa marafiki zake watano kuwa daktari wake alimwambia kuwa hataweza kufikisha mwezi julai hivyo asifanye mipango ya muda mrefu. Alielezwa kuwa akifikisha mwezi julai basi yeye ana bahati,” Jeff Koinange alieleza. 

Soma hadithi nyingine:

Viongozi kibao nchini wameweza kutuma risala zao za rambirambi akiwemo kiongozi wa upinzani Raila Odinga, Uhuru Kenyatta, William Ruto na Moses Wetangula.

View Comments