unnamed (3)

Katika kile kinachotafsiriwa kama mazao ya salamu "handshake" kati ya kiongozi wa taifa Uhuru Kenyatta na viongozi wa upinzani nchini, Uhuru amempa kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka kazi ya kuwa mjumbe maalum katika juhudi na mchakato mzima wa kuleta amani nchi ya Sudan Kusini.

Pata uhondo hapa:

Wizara ya maswala ya kigeni jana jumanne imechapisha kauli kuwa kiongozi huyu wa chama cha Wiper atahusika katika zoezi kuu la kurejesha hali ya utulivu na amani katika nchi jirani ya Sudan kusini.

"Uteuzi huu ni mojawapo ya juhudi za Kenya kuzidisha kuleta maendeleo ya pamoja katika kanda hii kwa kiujumla na pia kutafuta suluhu la kudumu kuhusu amani na usalama Sudan Kusini." ilisoma kauli hiyo katika chapisho la wizara ya maswala ya kigeni. 

Kalonzo sasa amekuwa kiongozi wa pili wa upinzani kupata shavu kutoka kwa serikali ya Uhuru Muigai Kenyatta baada ya mheshimiwa Raila Odinga kutangulia kuwa mjumbe maalum  maswala ya miundo misingi katika umoja wa mataifa barani Afrika.

Pata uhondo hapa:

Uteuzi huu umefanyika kipindi na ambapo Rais wa Sudan kusini Salvar Kiir yupo nchini katika ziara rasmi ya kumtembelea mwenzake Uhuru Kenyatta. Katika kikao kilichofanyika katika ikulu jumatatu, Rais Kenyatta aliuomba uongozi wa Sudan Kusini kukumbatia amani nchini humo ili wasadie kuzidisha kasi ya utangamano na maendeleo katika kanda ya Afrika Mashariki.

Ukizingatia kuwa tamasha ya kusherehekea uhuru wa nchi hiyo unakaribia, Rais Kenyatta amesema kuwa ni wakati mwafaka kwa wazalendo nchini humo kuonyesha uwepo wao katika upeo wa kitaifa, kanda nzima, barani afrika na kimataifa.

"Uongozi wa Sudan kusini una nafasi kubwa zaidi ya kuunda na kuwezesha mbinu zitakazopelekea kuimarika kwa amani pamoja na kutengeneza mazingira mazuri ili nchi ikue kiuchumi na utangamano mwema kati ya raia wake." Uhuru alimwambia Kiir.