- jah cure 2
- jah cure
- jah cure 1

Msanii mashuhuri wa Jamaica, aliyetarajiwa na ma elfu ya wakenya, Jah Cure tayari amewasili nchini kuwatumbuiza wapenzi wa reggae siku ya Jumamosi.

Ndege iliyombeba mkali huyu, iliwasili majira ya saa tatu usiku, siku ya Jumatano huku akiwa na wingi wa furaha na mbwembwe tayari kuwakilisha kwa mara nyingine tena.

Jah Cure atakuwa nchini kwa siku kadhaa ambapo anapaniwa kutumbuiza wakenya katika tamasha la Umoja, katika bustani la Uhuru, Nairobi Jumamosi.

Kabla ya hilo, mwimbaji huyo wa unconditional love, atakutana na wakenya na kufanya shughuli kadhaa za kusaidia jamii.

Waandalizi wa tamasha hili wamewahakikishia wakenya kuwa wakenya wataishi kukumbuka mpango huu kwa miaka kadhaa ijayo.

Tazama picha zifuatazo.

View Comments