- 60833513_2488872561145805_1398535902965953406_n (1)
- tanasha
- 66113340_653640925104835_5554398612772666647_n (1)

Dadaake Diamond Esma Platnumz, mara nyingine anamiminia mpenziwe Diamond Tanasha sifa.

Akizungumza na Wasafi FM, Esma kuwa Tanasha ni tofauti na wapenzi wa Diamond wa kitambo.

Haya alisema akichukulia hila  wapenzi wake Diamond wa hapo zamani, wakiwemo, Zari Hassan na Hamisa Mobeto. Aliongeza na kusema kuwa Tansha hapendi mtandao wa kijamii.

"Yeye ni tofauti. Haipendi mambo mengi anaweza kaa hata wiki mbili bila kuchapisha kwenye vyombo vya habari vya kijamii. Ikiwa ni mtu mwingine, tungekuwa tuliona hata choo, tungekuwa tumeona kila kitu katika nyumba yao."Esma alisema.

Maneno ya Esma yalikuja baada ya Diamond na Tanasha kusema jinsia ya mtoto wao ambaye wanamtarajia.

Haya yalitokea katika sherehe ya kuzaliwa kwao Tanasha na mamake Diamond Sanura Kasimu.

"Mpenzi wangu Tanasha ana mtoto wangu. Soini maana ya kuficha mambo hayo, "Diamond alisema, akiongeza kwamba Tanasha ana mimba saba miezi.

Diamond pia aliwazawadi mama yake na Tanasha gari mpya aina ya Toyota.

View Comments