CS MUCHERU

Makampuni ya ubashiri sasa yanaongoza katika mapato ya vyombo vya habari kupitia matangazo ya kibiashara.

Ripoti kuhusu hali ya vyombo vya habari nchini yaonyesha kuwa makampuni ya ubashiri na kuwekeana dau yilichangia 0.3% ya matangazo ya kibiashara katika vyombo vya habari kipindi cha mwaka 2014 lakini sasa makampuni hayo yameongeza matangazo yao hadi 22%.

“Kuongezeka kwa matumizi ya fedha katika matangazo ya biashara kumechangiwa na ushindani na kuongezeka kwa wahudumu katika soko la humu nchini,” ripoti iliyotolewa na TIFA na Reelforge ilieleza. Ripoti hiyo pia yaonyesha kuwa mashirika yalipunguza pesa za matangazo ya biashara mwaka 2018 ( bilioni 91.5) ikilinganishwa na mwaka 2017 (shilingi bilioni 108).

Kampuni ya Safaricom iliongoza katika matangazo ya biasahara miaka ya 2014, 2015 na 2016. Kampuni hiyo ilitumia shilingi bilioni 8.08 mwaka 2014, shilingi bilioni 7.42 mwaka 2015 na bilioni 6.42 mwaka 2016.

Mwaka 2017 serikali iliongoza katika mashirika yalioweka matangazo ya biashara kwa kima cha shilingi bilioni 8.64 ikifuatwa na Safaricom iliyotumia shilingi bilioni 8.12.

Mwaka 2018, “Tatua” ambayo ni kampuni ya kuwekeana dau iliyongoza katika matumizi ya pesa kwa matangazo ya biashara kwa kima cha shilingi bilioni 5.36 , ilifuatwa na Safaricom kwa kima cha shilingi bilioni 4.97.

Safaricom hata hivyo inaongoza katika matumizi ya pesa kwa matangazo ya biashara mwaka 2019, ikiwa tayari imetumia shilingi bilioni 9.71 kati ya mwezi Januari na Machi mwaka huu.

Radio bado inaongoza katika vyombo vya habari vinavyotafutwa kwa matangazo ya biashara licha ya kushuka kwa wanaosikiza radio kutoka asilimia 92 mwaka 2017 hadi asilimia 66 mwaka 2019.  Katika matangazo ya mabango katika kaunti ya Nairobi, Kampumi ya Pombe East African Breweries iliongoza, huku pombe aina na ya Guinnes na Tusker zikiongoza katika kutangazwa.

View Comments