Easy Come Easy Go: ‘Githeri man’ arejelea hali yake ya uchochole.
Martin Kamotho alias Githeri man alijipa umaarufu wakati wa uchaguzi mkuu wa 2017 alipopigwa picha akiwa kwenye foleni ya kupiga kura huku mkononi akijihami kwa mfuko wa plastiki uliokuwa na chakula chake –Githeri .Hakutaka kufanya kimoja kabla ya kurejelea kingine na ‘busara’yake hiyo ikamletea mazuri .Kando na kuangaziwa pakubwa na vyombo vya habari ,baadaye Kamotho alizawadiwa na watu binafsi na hata kusifiwa na wengine .
Maisha yake ya umaskini yalionekana kumwaga kwa sababu alialikwa kwenda Ikulu kupokea tuzo ya Head of State Commendation (HSC), na pia akatunukiwa shilingi laki moja .
Awali kabla ya umaarufu wake alikuwa pia na tatizo la kunywa pombe na mambo yalionekana kubadilika huku wengi wakitaraji angeuitumia fursa hiyo kubadilika na kujiboresha . Kampuni kadhaa zilimtumia ili kuangaziwa kwa kutoa ahadi ambazo nyingi hazijatimizwa .Kamotho anasema kwa jumla alipewa shilingi 150,000 lakini pesa hizo zimemfanya hata kuwa maskini zaidi kwani hakuna aliyetoa suluhisho la kudumu kumnasua kutoka umaskini .
Baadaye kwa ajili ya uraibu wa kunywa pombe alijipata katika kituo cha kumsaidia aache ulevi cha Mama Care Rehabilitation Centre, Kiambu. Rais Uhuru Kenyatta alihudhuria hafla hiyo ambapo Kamotho na wengine 77 walihitimu .Lakini cha kuvunja moyo sasa ni picha inayosambazwa mtandaoni akiwa anakokotwa katika toroli ,akionekana kuwa mlevi . Huenda jamii haikumsaidia Githeri man kwa kumpa alichohitaji au labda hajapata busara ya kuamua kujisaidia mwenyewe .