Holy Herb:Ajuza mwenye umri wa miaka 83 akamatwa na Bangi Nyeri
Ajuza mmoja mwenye umri wa miaka 83 aliyepatikana na gramu 600 za bangi amekiri mashtaka ya kuwa na bangi katika mahakama ya Nyeri . Lydia Mumbi alikamatwa na bangi hiyo yenye thamani ya shilingi 500 katika eneo la Mthinga ,Tetu . Bikizee huyo atasalia katika seli hadi jumatatu wakati atakapofikishwa tena kortini baada ya maelezo zaidi kuhusu kesi yake kufahamika .
Kwingineko polisi huko kakamega wamewakamata wanafunzi 19 waliopatikana na misokoto kadhaa ya bangi na pombe haramu . kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya muamis mashariki Joseph Ongaya amethibitisha kukamatwa kwa wanafunzi hao wa shule ya upili ya Mwitoti . Mwalimu mkuu wa shule hiyo ndiye aliywafahamisha polisi ,ambao walifaulu kuwakamata wanafunzi 19 ambao walihojiwa kwa siku mbili na makachero kuhusu tukio hilo . mabunda kadhaa ya miraa na sacheti zenye pombe haramu pia vilipatikana kutoka kwa wanafunzi hao .
Gavana wa kaunti hiyo Wycliffe Oparanya awali alikuwa amehusisha ongezeko la matumizi ya mihadarati na kuongezeka kwa visa vya uhalifu pamoja na biashara haramu ya uuzaji wa pombe haramu kwa wanafunzi wa shule za kaunti hiyo .