11 July 2019 1 Min Read
LO! Pozze pia asaka mke
by Albanus Kiswili Habari
Mwanamziki maarufu nchini kenya, Willy Paul amewaomba wakenya wamweleze mambo muhimu unayofaa kuzingatia ukitafuta mke. Pozze kwenye akaunti yake ya Instagramu amedai kuwa anamtaka mke ila hajui achague yupi.
"What are the qualities ofΒ a good woman?Niambieni maana hapa wapo wengi wanangoja mkuno ila sijui wa kweli jamani," Willy paul aliuliza.
Willy paul sasa ni msanii wa pili kuenda peupe kusema kwamba yuasaka mke mwema baada ya Ringtone kuanzisha viroja na sarakasi za kutafta mke. Jambo hili linajiri baada ya mjadala kuibuka kuhusiana na madai kuwa huenda Pozze alizipa nyimbo za injili talaka na sasa anaogelea katika raha za dunia.
View this post on InstagramA post shared by (@willy.paul.msafi) on Jul 2, 2019 at 2:26am PDT