Waluhya Waliwakosea nani? Vijembe 10 vya utani ambavyo vimetupatia Ucheshi
Kenya ,ni taifa zuri na lenye mvuto wa kipekee ambao hata wenyeji ,wakati mwingine tumejipata kuwa na fahari sana kuitwa wakenya .Jamii zetu mbali mbali pia zimechangia kuifanya nchi hii kuwa spesheli .Kutokana na maumbile tofauti ,tabia na mienendo mbali mbali ya jamii za Kenya ,mseto huu wa kila aina ya jambo ndio unaotufanya kuwa Wakenya .Lakini endapo kuna jamii ambayo imefanyiwa soga sana mtandaoni kwa njia nzuri na ya utani ili kutuchekesha sote,basi ni jamii ya waluhya . Aghalabu utani huu huhusisha mambo ya mlo . Baadhi ya vijembe hivi ni vitu vya kila siku vyenye msingi wa dhana potovu ama kiasi Fulani cha ukweli .Mengine yanatufanya tutafakari uhalisia wa maishaya kijamii ya makabila yetu na mengine yanatufanya tuwaze hata zaidi .Mengi hata hivyo ni ya kweli na yanakwaza . Hii hapa orodha ya vijembe 10 vya utani kuwahusu waluhya ambavyo vimetupa tabasamu hata tunapokabiliwa na nyakati ngumu .
1.Kumeza sausage /smokie kama capsule
Now.Najua kuna soga za kutuchekesha ,na tunaweza kujaribu kutafakari inavyowezekana ,lakini iwapo unajua capsule na jinsi dawa inavyomezwa –hebu fikiria kuchukua soseji ikiwa nzima halafu uipurukushe kinyuani.Matokeo yatakuwa kitu kingine.utasakamwa lakini apparently jamii moja tu ndio iliyo na uwezo wa kufanya hilo .I surrender .
2. Mluhya akila kuku ,anakula vyote, sauti na kivuli!
Hii hata sitaeleza zaidi . Imetosha tayari jinsi ilivyo lakini nimechukua muda mrefu kufirikia jinsi unavyoweza kula sauti ya kuku au hata unavyotayarisha kivuli cha kuku kuwa mlo .I give up .
3.Papa shirandula na Patanisho .
Hapa najua kuna tone la ukweli .Nimeskia utani huu eti ukitaka msichana mluhya akupende kupindukia ,usiku mfungulie atazame papa shirandula akinyofoa sima na kuku .Asubuhi mfungulie radio Jambo asikilize Patanisho ya Gidi na Ghost.Wiki moja baadaye panga harusi ! You are already romantic…. Kali sana .
4 Gani tamu kati ya ugali na Keki ?
Umesikia utani huu wa rafiki ambao wapo njia panda kuhusu zawadi ya kumpa rafiki yao mluhya.wakisema eti keki haitamridhisha na badale yake sima ndio zawadi tosha .Mluhya hujamridhisha endapo hajakula sima . Inasemekana ni dharua kubwa sana kumpa mwanamme mluhya wali kama chakula,hiyoni snack ama kiamsha hamu tu. Vitu kama spaghetti ni mzaha sana kwa mluhya !
5.Dem yako hushiba ama ni mluhya?
Hii imekuwa ikibadilishwa kila uchao ili kutoa taswira mbali za kuvunja mbavu.Sijui ni mtani yupi huyu aliamua kuja nah ii lakini najua umezisikia au kuzisoma .Mengine ya kuchekesha ni maswali kama-Chali yako hukupea pesa za salon ama ni mluhya ? Boyfriend yako ni babyface ama ni mluhya?
6.Unga,Posho mill na Sima
Hizi najua wengi mmeziona kuanzia jadi . Nimeona tangazo bandia la nyumba ya kukodi ambalo limeongezwa chumvi ili kusoma hivi - A spacious Bedsitter,inbult wardrobes and a poshomill nearby.Ideal for luhyas! Jamani najua waluhya wanapensa ugali ,lakini hebu fikiria kuhusu mtu ambaye anaweza kuchagua nyumba ya kuishi kwa msingi wa owepo ya mashine ya kusaga mahndi au nafaka . Kisha kuna hii moja yenye picha ya bundi aliyefurahi na maandishi – kale kafeeling ka mluhya akisikia patanisho alafu advert ya Unga iwe next’.
Wengine wameizidisha na kuweka utani kama ; Breaking News,Man dies after attempting to speak luhya language with an empty stomach . Halafu kuna hii nyingine – Ukipika ugali kubwa na mayai mawili ,inafika point unachuna ugali na unapoint mayai …
Siwezi kusahau picha za utani zilizoonyesha mtu aliyedaiwa kuwa mluhya ambaye alikuwa amezirai ,lakini pindi tu alipowekewa sima karibu na pua ,aliamka papo hapo !
7.Chai .
Hii ni ya tangu jadi . umeskia mtu akinywa chai anaulizwa - kwani wewe ni mluhya? Cha kuchekesha ni kwamba najua watu wengi hata wasio waluhya wanaopenda chai .Sijui aliyeitunga hii alifanya utafiti gani lakini imetamba sana . Kisha kuna ule utani wa mluhya aliyeanza kuchemsha maji ya kuoga lakini kati kati akabadilisha mawazo na kuweka majani ili iwe chai .
Pia kuna nyingine ya mluhya kulamba sukari na kunusa kahawa ndio apate feeling ya ‘breakfast’.
- Mazgwembwe
Hii najua mumeshaisikia na kuhusu miguu ya waluhya iliyojaa,sehemu ijulikanayo kama ‘mazgwembe’ . nikapata kuiona moja kwenye twitter mtu akiuliza - Kwa nini waluhya hawananga pole dancers?
Mtu akajibu –
Hizo mazgwembe zao zitaangusha pole .
Hilo limeashiria maumbile ya kipekee ya waluhya walio na miguu minene na yenye nguvu .Najua waluhya ambao huitwa jina la utani ‘Stunya’.
- Matamshi ya B na P na D na T
Kila jamii ina athari Fulani ya kimatamshi kwa sababu ya muingilio wa lugha ya mama .waluhya hawajasazwa hapa na umesikia aghalabu watu wakiwaambia waluhya kuhusu kinachoonekana kama visawe katika matamshi yao.
Sio purupuru ni buru buru
Sio matako ni ‘madhako’
Sio Tisco ni Disco
Kisha hii -
Saa hii Kuna mluhya anajua ati Pope Collymore,Pope Marley na Pope Francis ni mabro . Ukatili!
10.Shortest Prayer
Mengi yamesemwa ,na mengine zaidi kuandikwakuhusu wahubiri waluhya na jinsi walivyo na passion katika kazi yao ya mahubiri . Imedaiwa kwamba wengi wa wahubiri hawa huomba kwa muda mrefu hadi kuwachosha waumini .Lakini siwezi kusahau soga moja iliyozuka kuhusu jinsi ya kumfanya mhubiri wa kiluhya kufupisha maombi wakati wa hafla .Siri imesemwa aktika utani huo ni kuhakikisha kwamba baada ya chakula kuwekwa mezani,hakikisha kwamba bakuli iliyojaa monofu ya kuku inaweza mbali sana na mhubiri . kwa sababu ya pupa ,atafupisha maombi yake ili kuharakisha na kukimbilia ile bakuli na kuivuta upande wake! Huu ni ukatili .
Tuambie ,ni vijembe vipi vya kuvunja mbavu ambavyo umeviona au kusoma mtandaoni ?