- 65505946_2402850666615288_205768720042353059_n (1)
- 66649011_142309356957440_3882990979081429845_n
Babake Diamond Platnumz, Abdul Juma hatimaye alikutana na mamake Diamond siku ya Jumapili katika sherehe ya kuzaliwa kwake kule Milimani.
Wawili hawa hawakuelewana hadi hivi karibuni, wakati ambapo Diamond alikubali kufadhili bili za matibabu ya baba yake.

"Ninafanya vizuri na afya yangu ni bora. Sikuweza kuvaa viatu lakini sasa ninaweza," Juma aliiambia vyombo vya habari vya Wasafi.

http://Diamond ashambuliwa na watu kwa kumzawadi mamaye na mpenziwe na kumwacha babaye
Wazazi wake Diamond waliachana hapo awali na wote wawili wameendelea na maisha yao. Mamake Diamond ana uhusiano wa kimapenzi na Rally Jones, naye
baba yake ana familia nyingine.

"Mimi sihisi wivu kwa kuwa mke wangu aliendelea na maisha yake lakini ninaomba Mungu kwamba anaishi kwa furaha," Juma alisema.

Alimshauri asiskize kile ambacho watu wanasema lakini badala yake kuzingatia maisha yake.

Alipoulizwa ni zawadi bora gani aliyokuwa nayo kutoka kwa mke wake wa zamani, Juma alisema kuhudhuria siku ya kuzaliwa kwake ni zawadi kubwa zaidi  kwani
hapo awali hakualikwa.
soma mengi hapa
/