Bwana samson, 32, aliomba kupatanishwa na mkewe Elizabeth,30, ambaye tangu waoane wamekuwa na matatizo ya chumbani. Samson anasema kuwa mkewe amekuwa mkali kama chui kila wakati anapotaka kushiriki naye ngono. Kulingana naye Samson, bibiye alikuwa anamkzaia tendo la ndoa.

"Mke wangu amekuwa mkali sana kila ninapotaka tendo la ndoa na hasa hivi majuzi. Tumekuwa kwa uhusiano huu kwa miaka miwili sasa. Tumekuwa na matatizo kidogo kidogo kuhusu tendo la ndoa kwa miaka yetu miwili ya uhusiano."

Bwana Samson alisema kuwa mkewe amekuwa mkali kama simba jike. Hata hivyo, wawili hawa hawana mtoto licha ya kuwa wamekuwa na uhusiano kwa miaka miwili sasa. Bwana Samson akisema na radio Jambo anasema kuwa bibiye alirejea kwao siku ya Jumatatu.

"Nilipotoka shughuli zangu nilipata kama amekwisha funganya virago vyake na akaondoka. Jana jioni alinieleza kuwa anataka niende kwao."

Samson alisema kuwa hajawahi kuwatembelea wazazi wake Elizabeth ila alikuwa anazungumza na babaye Elizabeth kwa njia ya simu kwa miaka miwili sasa. Bwana Samson alieleza kuwa  anawajua dada na ndugu zake Elizabeth.

"Nilizungumza na babake kwa njia ya simu na babaye akanieleza kuwa atakuja kunitembelea."

Juhudi za radio Jambo za kumfikia bibiye Samson ziligonga mwamba.

Samson alimwomba mkewe arejee nyumbani waweze kusulihisha matatizo yao na kisha waendeleza maisha yao ya kila siku.