KOIMETT

Esther Koimet, katibu wa kudumu katika wizara ya uchukuzi, amekuwa akipigiwa upatu kutwaa wadhifa wa waziri wa fedha kujaza nafasi ya Waziri Henry Rotich ambaye anakabiliwa na mashataka ya ufisadi.

Kwa sababu waziri mpya anahitaji kupigwa msasa na kuidhinishwa na kabla ya kuteuliwa rasmi, ikulu ya rais ilikuwa jana jioni ikitafakari kumtaja waziiri wa uchukuzi James Macharia au mwenzake wa Jumuia ya Afrika mashahriki na ustawi wa kanda hii Adan Mohamed kama kaimu waziri.

"Kuna dharura ya kujaza nafasi hii kwa hivyo tarajieni tangazo wakati wowote ule," katibu mmoja wa kudumu alisema.

Rais Uhuru Kenyatta kulingana na watu wa karibu naye amekuwa akishauriana na wadau mbali mbali kuhusu kujaza pengo hilo punde tu Rotich alipokamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma za ufisagdi.

Vita hivi vya ufisadi vinavyo husisha shilingi bilioni 63 za ujenzi wa mabwawa mawili, vimehusisha maafisa wakuu watano katika wizara ya fedha akiwemo waziri Henry Rotich na katibu wa kudumu Kamau Thugge.

Wengine ambao pia walishtakiwa ni mwanauchumi na mkuu wa idara ya maswala ya kifedha ya ulaya Kennedy Nyakundi, mkurugenzi wa ukusanyaji wa raslimali katika wizara ya fedha Jackson Njau na inspekta mkuu wa mashirika Titus Muriithi.

Koimett aliye na tajiriba ya zaidi ya miaka 25 katika serikali, alionekana kuongoza orodha ya wale wanaopigiwa upatu kuchukuwa mfasi hiyo.

“Rais anataka mtu mzoefu na mwenye kuaminika,” duru karibu na mashauriano ya rais zilisema. Koimet ambaye alizaliwa mwaka 1967, ana taaluma ndefu katika utumishi wa umma, akihudumu kama katibu wa kudumu katika wizara ya Utalii na habari na kama meneja mkurugenzi wa Benki ya akiba ya Kenya Posta.

View Comments