Mwanamme mmoja mwenye umri wa makamu amezuiliwa katika kituo cha polisi cha serem kwa tuhuma za kujidai kuwa afisa wa shirika la NEMA kaunti ya Vihiga.

Kwa mujibu wa chifu wa Shaviringa bi.Josephine Khalwale ni kuwa mwanaume huyo anayekisiwa kujitambulisha kama George Kirima wakiandamana na wenzake watatu, walikuwa wamevamia duka moja eneo la Shaviringa kwa madai ya kufanya msako wa mifuko za platiki na hatua iliwavutia wenyeji na kupelekea kukamatwa kwake huku wenzake wakitoweka ndani ya gari ndogo walilokiwa wakitumia.

Naye kwa upande wake afisa mkuu wa NEMA kaunti hiyo bw. Jasper Omwenga akisisitiza kuwa kama shirika watahakikisha kuwa hatua za kisheria zimechukuliwa dhidi yake.
Mshukiwa huyo anatarajiwa kufikishwa katika mahaka ya hamisi hapo kesho.