Mama Shantel alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Sam akisema kuwa walitengana baada yake kushuku kuwa ana uhusiano na boss wake.

"Ilikuwa ivi, tumeenda nyumbani kulala na katika harakati ya kusoma katiba nikasema nimechoka, kuniuliza mbona nimechoka akalalamika mbona nimechoka baadaye akaenda jikoni na akaja akanimwagia maji ndoo mzima.

Baada ya bedroom ku loa maji nikaenda kulala chumba cha watoto na baadaye akaja na kunitandika na hapo nikaondoka." Alieleza.

Aliongeza,

Nimejaribu kuzungumza naye lakini kwenda kwa mtandao wake wa Facebook nikapata ameweka mwanamke mwingine. Kwa hasira nami nika download picha ya mwanaume aliyenishuku naye na nikaweka profile picture whatsapp na hapo akasema nafaa niendelee na umalaya.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka tisa.

Bwana Sam alipopigiwa simu alisema,

Unajua kuna mahali alikuwa anafanya job na kuna jamaa alikuwa na urafiki naye ambaye alikuwa ameoa na alikuwa akija hata penye tunaishi.

Saa zingine akiwa job alikuwa anamuita, saa zingine anatoka kwa nyumba saa moja anarudi hadi saa mbili sijui anapeleka pesa wapi. Alinitoka na alinikosea kabisa." Mumewe mama Shantel alisimulia.

Isitoshe alisimulia kuwa walipogombana na mkewe kuondoka yule jamaa alikuwa analala kwa ile nyumba kwani hata mwenye nyumba alimweleza.

''Mimi siwezi chota kisima ambacho mwingine anachoka kwa hivyo wacha aendelee kuchota." Alisema bwana Sam huku akishikilia wawili hao hawatarudiana.