Gavana wa Nairobi, Mike Sonko amewarai wabunge vijana kuendeleza mswada aliokuwa marehemu Ken Okoth wakuhalilisha bangi nchini Kenya.

Akizungumza katika hafla ya misa ya wafu ya Okoth katika shule ya St. Mary's Nairobi.

Sonko aliwarai wabunge hao ikiwemo, John Kiarie mbunge wa Dagoretti kusini, Babu Owino mbunge wa Embakasi mashariki na Charles 'Njagua' Jaguar mbunge wa Starehe kuhakikisha mswada huo umepitishwa.

Kulingana na Sonko ni kuwa anaamini kuwa bangi ina uwezo wa kuponya ugonjwa wa saratani na itawasaidia wengi kama itahalilishwa.

"Huyu ndugu yetu Ken Okoth alitaka kulegalize marijuana ama bangi na tunasikia bangi iko na dawa ya cancer. Mheshimiwa Babu Owino na wale wabunge vijana wako hapa, kina KJ kina Jaguar msiwache hiyo kazi nzuri ya mheshimiwa Ken Okoth iishie hapo.

Endeleeni na hiyo mswada bhangi ikuwe legalized." Alisema Sonko huku wananchi waliofurika katika shule ya St. Mary's wakishangilia.

View Comments