01 August 2019 1 Min Read
Picha ya siku: Je hii ndio jinsi mpya ya kumsalimu mumeo?
by Brian Ndungu Habari
Picha ya bi Rachel Ruto, akimsalimu mumewe naibu wa rais, mheshimiwa William Ruto, imekuwa chanzo cha mazungumzo mengi katika mitandao ya kijamii.
Katika picha ile, bi Rachel anaonekana akiwa mnyenyekevu mno kwani anamsalimu mumewe huku akiwa ameinamisha kichwa chake na mkono wake wa kushoto ukiwa umeshikilia wa kulia. Hii yote ni kuashiria heshima kuu sio tu kwa mumewe bali pia kwa kiongozi.
Je wadhani hii ndio jinsi wake wanapaswa kuwasalimu waume zao?