Baba Fanwell alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe mama Fanwell akidai kuwa mkewe amepotea kwa mda wa mwezi mmoja sasa.

A man is born to suffer my friend alisema baba Fanwell.

"Huyu mwanadada nilimpea moyo wangu wote lakini ameniumiza sana. Huyu mwanadada tumejuana miaka kumi na tumezaa watoto watatu na sijui ni shetani mgani amemuingilia kwani kila baada ya miezi mitatu hutoroka na kuwacha watoto." Alisema.

Aliongeza,

Nikakwambia yale tumekosana naye unaweza shangaa. Kwa mfano hajakuwa akifurahia niki support mtoto wa ndugu yangu kimasomo kwa hivyo ni mambo ya pesa. La pili ni kama wamama wanamchocha sana.

Mama Fanwell alisema kuwa mumewe ana familia lakini anaweka fikra zake kwingine na angependa kuwa awe na balance fulani. Isitoshe akiwa na makosa yeye huwa haelewi.

"Nilipokasirika na kumwambia nataka kuondoka hapo akanipiga na kuniumiza kifua." Alielezea.

Alipoulizwa kuhusu yale, bwana Geoffrey alisema hakumpiga ila alikuwa anamzuia asibebe nguo zake na katika ile harakati akamzaba kofi moja.

Aliongeza, amesema alikuwa amenipa moyo wake lakini pia mimi singeishi naye kama singekuwa nimempa moyo wangu. 

Mama Fanwell alisema atampa mumewe miaka miwili ajirekebishe akisema hamchukii ila anachukia ka shetani kaliko kichwani chake.