Gloves are Off! Ruto apuuza BBI ya Raila na Uhuru
Naibu wa rais William Ruto ametuma ujumbe katika twitter unaoonekana kupiga vijembe juhudi za Kiongozi wa ODM Raila Odinga na kiongozi wa walio wengi bungeni Aden Duale kwa kujadili BBI na Punguza Mizigo mtawalia . Kupitia ujumbe huo Ruto amewakemea vikali wanaojadili miswada wa Punguza Mizigo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2022 .
Jopo la Building Bridges Initiative liliundwa baada ya mwafaka wa ‘handshake’ kati ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila odinga . Raila mwezi uliopita alipuuza mswda wa punguza mizigo na kuwaraia wakenya kungoja ripoti itakayotolewa na jopo la BBI. Wakati huo huo Duale wameunga mkono wazi kurekebishwa kwa katiba ili kubadilisha mfumo wa serikali .
Mbunge huyo wa Garissa mjini amesema ataunga mkono pendekezo la serikali yenye utawala wa bunge lenye maamlaka il kumaliza ghasia za kila mara wakati wa uchaguzi wa urais . ODM ilikosoa mswada wa Punguza Mizigo ikitilia shaka jinsi tume ya uchaguzi IEBC ilivyothibitisha uhalali wa sahihi zilizokusanywa hasa baada ya juhudi kama hizo chini ya mpango wa Okoa Kenya mwaka wa 2017 kufeli wakati muungano wa CORD uliposhindwa kupata sahihi halali zilizohitajika .