1585060

Kijana wa miaka 13, wa darasa la 7 kutoka shule moja ya Kasuku, Ol Joro Orok, anapigania maisha yake katika hospitali ya J.M.Memorial, Ol Kalou huku akiwa na majeraha mabaya ya kichwa, mkono na pia mguu.

Kijana huyo alidhulumiwa na babake mwenye umri wa miaka 47 siku ya Jumatatu sababu kuwa alifukua viazi kadhaa kabla ya kupika na kuvila. Tukio hilo lilitokea nyumbani kwao Kihingo, Kasuku.

Mamake kijana huyo ambaye walitengana na babake miezi kadhaa iliyopita, anahofia maisha yake kila siku kwani amekuwa akimtishia. Kufuatia kisa hicho, sasa anahofia mumewe anaweza mtafuta na amuue.

Alisema kuwa ndugu zake kijana yule walimpeleka mwanawe hadi anakoishi katika maeneo ya Kasuku siku ya Ijumaa. Hali yake haikuwa njema na hapo akamkimbiza katika hospitali ya J.M Memorial.

J.M.Memorial hospital Medical Superintendent, Dr.Joram Muraya, this evening confirmed the pupil is admitted at the facility.

Jane Njeri, mamake kijana yule sasa anaitaka serikali imtie nguvuni Waiguru King'ori ili aweze kutulia na kuwatunza wanawe huku akiomba msaada kutoka wasamaria wema.

Alipopigiwa simu, KIng'ori alikana kuwa Njeri ni mkewe lakini alisema kuwa anatafuta vijana wake watatu ambao walitoweka kutoka nyumbani kwao baada ya kuwatuma kwenda shambani kuendea malisho ya ng'ombe.

Mkuu wa polisi kutoka kituo cha polisi cha kaunti ndogo ya Nyandarua West Sub-County, Isaac Ruto, alisema kuwa kesi hiyo iliripotiwa katika kituo cha Polisi cha Kasuku jana jioni.

Alisema polisi watahakikisha kuwa jamaa huyo amekamatwa na pia kijana huyo kupata haki.

-Ndichu Wainaina

View Comments