- IMG_20190815_130627[1]__1565879038_27018
- IMG_20190808_112922[1]__1565258684_65005 (1)

Kituo chako mahabubu cha Jambo kwa mwezi mzima sasa kimejikita katika mchakato wa kuwatunuku wasikilizaji na hela lukuki. Zoezi hii ilianza tarehe 15 Julai na linatarajiwa kufungwa tarehe 30 Agosti mwaka huu.

Soma hapa:

Cha msingi sonko huyu anahitaji kujua ni iwapo wasikilizaji wanaelewa kabisa maneno machache yanayolipa pesa “The Phrase That Pays”. Iwapo shabiki ataweza kung’amua Redio Jambo Ongea Usikike, sonko huwatuza shilingi 1,000. Aidha, mashabiki wanaozidisha ubunifu na kuyaandika maneno hayo katika bango hutunukiwa shilingi 5,000 pesa taslimu.

Juma lijalo sonko huyu atazamia mji mkuu wa Nairobi kuwazawadi mashabiki. Sonko wa masonko atatembea viunga vya Nairobi kwa mara nyingine kwa udi na uvumba kumsaka atakayeng’amua The Phrase that Pays ambayo ni Redio Jambo Ongea Usikike.

Soma hapa:

Mapokezi makubwa hii leo yameshuhudiwa Voi, Taveta na Kibwezi huku wasikilizaji wakipata zawadi kemkem kutoka kituo hiki.

View Comments