15 August 2019 1 Min Read
Wanafunzi waliopatikana na dawa za kulevya waachiliwa kwa dhamana
by Brian Ndungu Habari
Mahakama mjini Voi kaunti ya Taita Taveta imewaachilia kwa dhamana wanafunzi wawili kati ya watatu waliokamatwa kwa madai ya kupatikana na madawa ya kulevya.
Hakimu wa Voi Ann Karimi amewaachilia wawili hao, Jeremiah Shake na Ngure Kiroshi kwa dhamana ya shilingi laki mbili au pesa taslimu laki mbili, huku keshi hiyo ikiratibiwa kusikizwa Septembe 26.
Washukiwa wengine watatu waliokamatwa katika msako dhidi ya mihadarati katika kaunti hiyo bado hawajafikishwa kortini.
Kwingineko, wawakilishi wadi wa kaunti ya Taita Taveta wamekanusha madai ya kutaka kumng'oa mamlakani gavana Granton Samboja madarakani.
Kiongozi wa wengi bungeni Jason Tuja anasema kuwa kwa sasa nia yao ni kuwepo kwa mazungumzo kati ya pande zote mbili ili kumaliza mzozo unaoendelea kati ya bunge la kaunti na gavana Granton Samboja.
Amewataka wananchi kupuzilia mbali uvumi unaoendelea kwa mitandao ya kijamii kwamba bunge la kaunti lina nia kujadili msada wa kutokuwa na imani na Samboja.