Paul Pogba awapuuza mashabiki wanaombagua kirangi
Kiungo Manchester United, Paul Pogba amewakashifu watu wanaobagua wachezaji na watu wengine kwa madai ya rangi zao. Pogba alibaguliwa na mashabiki wa Manchester United baada ya kupoteza mkwaju wa penalti kwenye mechi dhidi ya Wolves iliyokamilika sare ya goli moja kwa moja.
"Jambo linalo ufanya Ulimwengu kuwa wa kupendeza ni uwepo wa rangi nyingi pamoja na tamaduni nyingi tofauti tofauti. Kwangu mimi binafsi ninapozungumzia suala la ubaguzi wa rangi nafifikiria kuwa huo ni upuuzi mtupu kwa sababu limekuwepo kwa muda mrefu."
"Mimi nayafurahia maisha yangu kwa sasa na ninafuraha kuendelea kucheza soka langu kwa sasa. Ninafuraha kila wakati ninapowafurahisha watu kwa madoido uwanjani ila hakuna siku nitamsikiliza yeyote anayenikashifu kwani najua mada yao kuu ni kuniangusha jambo ambalo sitokubali lifanyike."