msalaba

Polisi nchini Uganda inachunguza kisa ambapo mwanamume mmoja ameshambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa madai ya kuunga mkono chama tawala cha National Resistance Movement (NRM).

Baker Kasumba, anayesadikiwa kuwa na umri wa chini ya miaka 21 aliripotiwa kushambuliwa na watu wawili wasio julikana akitoka kazini kuelekea nyumbani katika eneo la Kalerwe siku ya Alhamisi.

Gazeti la Daily Monitor nchini Uganda limeripoti kuwa taarifa iliondikishwa na muathiriwa katika kituo cha polisi cha Kalerwe, inasema Kasumba alidai alishikwa kupigiliwa misumaru kwa nyundo na watu ambao hakuwafahamu kwa kuvalia kofia ya NRM ambayo huvaliwa na wanaharakati wa chama tawala.

https://twitter.com/DailyMonitor/status/1167083723663257600

Kulingana na taarifa hiyo maafisa wanasema muathiriwa alifungwa mikono pamoja alafu akawekewa kofia hiyo katikati ya mikono yake na kupigiliwa misumari kwa kutumia nyundo.

Bw pia ameripotiwa kueleza polisi kuwa waliomshambulia walimwambia tunakusulubisha ili ufariki kwa ajili ya chama anachokienzi

Naibu msemaji wa polisi mjini Kampala Luke Owoyesigyire, amesema kuwa polisi ameanzisha msako mkali kuwatafuta washukiwa.

Kisa hicho kimepokelewaje?

Kisa hicho kimezua gumzo kali katika mitandao ya kijamii huku baadhi ya wafuasi wa upinzani wakidai kuwa ni njama ya serikali.

Kashari Boy aliandika katika Twiiter yake akisema mhalifu ni mhalifu haijalisha anaunga mkono chama gani cha kisiasa.

-BBC

View Comments