Babake Diamond Platnumz aposti ngoma ya Harmonize. Aonywa kutengwa(Video)
Mzee wa Mondi amejipata kukosolewa na mashabiki wake baada ya kuchapisha video ya Harmonize katika mtandao wake wa insta. Kutoka Harmonize atangaze kuitema lebo ya WCB, stima za ushikaji zimekata ghafla. Ushikaji wa zamani wa kuposti kazi za msanii Harmonize hazionekani tena.
Soma hadithi hapa:
Harmonize mwenyewe aliposti ngoma ya Mbosso aliofanya na Reekado. Hali kadhalika, dogo alipost ngoma yake Rayvanyy Remix Tetema ila wawili hao hawakupost Inabana yake na Eddy Kenzo.
https://www.instagram.com/p/B1tI8VxgUZE/
Sasa mzee wa Diamond Platnumz huenda hajapata kuelewa upepo huu wa ubifu na anashobokea kazi za staa huyu kwenye mitandao ya kijamii.
"Mzee utatengwa π πππ π π, "alisema shabiki mmoja.
Soma hadithi hapa:
Huenda kuna baadhi ya vijisehemu katika mkataba vinavyombana kufanya kazi za nje na kutanua kama mzazi wake katika tasnia hii Diamond Platnumz.