Mwanamme aliyembaka ajuza mwenye umri wa miaka 80 katika kijiji cha  Kimoning huko Keiyo kusini amehukumiwa miaka  kifungo cha miaka 35 jela  na mahakama moja ya Eldoret .Hakimu mkuu Harrison Barasa   amempata na hatia  Benjamin Kiprop  ambaye  ana umri wa miaka 25 aliyetekeleza kitendo hicho tarehe  8 Julai mwaka wa 2017 .

Barasa amesema ushahidi uliotolewa na ajuza huyo kortini unaaminika . Aliiambia mahakama jinsi mshukiwa alivyouvunja mlango wake mwendo waa tano usiku akiwa amejihami kwa kisu .

Ameongeza kwamba Kiprop kisha alimbaka  mara  mbili na juhudi zake za kupiga kamsa ili aokolewe ziliambulia patupu kwa sababu Kiprop alikuwa amembana shingo. Ajuza huyo amesema nusra afariki na yungali hajapona kabisa kutoka na masaibu hayo .

View Comments